1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Demokrats yaashiriwa kushinda katika jimbo la Virginia.

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuZ

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa, chama cha Democrats kimepata nafasi ya kuongoza katika Baraza la Senet baada ya kupata ushindi kwa wingi wa viti kwenye uchaguzi wa Seneta katika jimbo la Virginia.

Ikiwa ushindi huo utathibitishwa utawapa nafasi chama cha Democrats usemi mkuu katika Bunge la Congress kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.

Mapema rais George W. Bush baada ya kushindwa vibaya chama chake alitangaza kujiuzulu kwa waziri wa Ulinzi Donald Rumsfeld.

Aidha rais Bush amemchaguwa mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi la Marekani CIA Robert Gates kuziba nafasi ya Rumsfeld.

Akitoa shukurani zake kwa waziri wa Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld kutokana na kazi zake alizozifanya, Rais Goerge W. Bush amesema.

“Utumishi wako umeifanya Marekani kuwa imara, na kuifanya Marekani kuwa taifa salama. Tutakukumbuka, na kunakutakia kila la Kheri wewe na Joyce katika miaka ijayo“.

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ikulu ya White house, Marekani amekiri kuwa sera zake nchini Iraq hazifanyi kazi inavyotakiwa ama kuleta manufaa.

Nancy Pelosi kutoka chama cha Democrats anatazamiwa kuwa mwanamama wa kwanza kushika wadhifa wa Uspika katika Bunge la Marekani, wadhifa ambao ni mkubwa katika chombo hicho.