1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Gates atawazwa rasmi waziri wa ulinzi Marekani

19 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCiM

Mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Marekani Robert Gates ameapishwa rasmi kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani akichukua nafasi ya bwana Donald Rumsfeld aliyejiuzulu mwezi uliopita.

Gates amesema atalipa kipaumbele suala la kuutatua mgogoro wa Iraq akionya kwamba kushindwa kuutatua mzozo huo kutasababisha hali ngumu kwa Marekani na kuihatarisha nchi hiyo kwa miongo kadhaa ijayo.

Gates amechukua wadhifa huo wa waziri wa ulinzi wakati ambapo kunafanyika mageuzi makubwa ya sera ya Marekani nchini Iraq.

Rais Gorge Bush wiki iliyopita alisema atasubiri hadi mwezi januari ujao ambapo atatangaza mkakati wake mpya ili kumpa nafasi bwana Gates aweze kutoa ushauri wake.