1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Karzai asema Taleban si chochote kwa serikali yake

7 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbO

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema kuwa wanamgambo wa Taleban hawaleti kitisho chochote katika serikali yake na kwamba kundi hilo limeshindwa.

Karzai alisema hayo baada ya mazungumzo yake na Rais George Bush Camp David kakribu na Washington.

Viongozi hao wawili pia walikubaliana kwamba hakuna makubaliano yoyote yatakayofikiwa na wateka nyara wa Kitaleban wanaowashikilia raia 21 wa Korea Kusini nchini Afghanistan.

Aidha Rais Bush kwa upande wake alielezea matumaini ya Marekani ya kuwakamata viongozi wa kundi la Al Qaida waliyojificha nchini Pakistan.