1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:kituo cha kijeshi cha Marekani kwa Afrika kuwekwa Ujerumani kwanza

8 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUB
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York MarekaniPicha: AP

Wizara ya ulinzi ya Marekani imeandaa mipango ya kujenga kitengo maalumu cha kijeshi kitakachoshughulikia bara la Afrika.

Marekani inapanga kwanza, kukiweka kitengo hicho katika mji wa Stuttgart kusini mwa Ujerumani kabla ya kukihamishia Afrika katika siku za usoni.

Kiasi cha dola milioni 50 kimetengwa kwa ajli ya mradi huo.

Rais G. Bush amesema kituo hicho kipya kitaimarisha ushirikiano baina ya Marekani na nchi za Afrika hasa katika harakati za kupambana na ugaidi.