1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON.Liberia kufutiwa deni

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSY

Marekani inatarajia kufuta deni la zaidi ya dola milioni 300 kwa nchi ya Liberia.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice ameyasema hayo katika mkutano wa wafadhili juu ya Liberia mjini Washington na wakati huo huo amezihimiza nchi za magharibi kuisaidia nchi hiyo.

Vita vya miaka minne vilivyoikumba Liberia viliharibu miundo mbinu ya nchi hiyo na pia kusababisha vifo vya takriban watu laki mbili.

Liberia inadaiwa na nchi za nje jumla ya dola bilioni 3.7.