1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:MacCain ajitupa uwanjani kusaka tiketi ya kuingia Ikulu ya White House

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNc

Seneta wa Marekani wa chama cha Republican John McCain ametangaza kujibwaga katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 nchini humo.

McCain mwenye umri wa miaka 70 ametoa tangazo hilo wakati akihojiwa katika kipindi cha maohojiano na televisheni ya Marekani ya CBS.

MacCain seneta wa jimbo la Harizona anaunga mkono mpango war ais Bush wa kuongeza wanajeshi wa Marekani nchini Iraq lakini pia amekuwa mkosoaji mkubwa wa waziri wa zamani wa Ulinzi Donald Rumsfeld.

Endapo atachaguliwa katika uchaguzi huo wa mwaka ujao basi MacCaina takuwa ndiye kiongozi mzee kabisa kuwahi kuchaguliwa kuingia ikulu ya White House.