1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Majeshsi ya Marekani kuondoka Irak?

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUO

Habari kutoka Washington zinasema kuwa huenda Marekani ikaanza kuondoa majeshi kutoka Irak kuanzia mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani bwana Robert Gates amesema hayo mbele ya kamati ya majeshi ya Seneti. Lakini ameleeza kuwa hatua hiyo itategemea na iwapo mkakati mpya wa kuleta usalama nchini Irak utafanikiwa.

Hapo awali rais Bush aliamua kuongeza wanajeshi alfu 21 nchini Irak.