1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani haijapata uthibitisho iwapo Korea ya kaskazini imeanza kufunga kinu cha nyuklia

18 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC98

Marekani imesema haijapata uthibitisho iwapo Korea ya kaskazini imeanza kuufunga mtambo wake wa nyuklia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ameeleza hayo kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba yumkini Korea imeshaanza kuufunga mtambo wake wa nyuklia wa Yongbyong.

Korea ya kaskazini ilipaswa kuanza kukifunga kinu chake cha nyuklia jumamosi kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa baina yake na jumuiya ya kimataifa.