1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani kurejesha uhusiano na serikali ya Palestina

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqR

Marekani na Umoja wa Ulaya zitarejesha uhusiano na serikali ya Palestina kwa kuiondolea serikali hiyo vikwazo na kuanza kuipa tena misaada ya fedha.

Akizungumza muda mfupi baada ya serikali mpya ya Palestina kuundwa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice ameahidi kuwapa wapalestina misaada kamilifu madhali, serikali hiyo mpya sasa haina wawakilishi wa chama cha Hamas.

Ili kutekeleza shabaha hiyo Marekani itaondoa vikwazo ilivyoweka hapo awali kufuatia ushindi wa chama cha Hamas katika uchaguzi.

Bibi Rice pia amesema Marekani inakusudia kuondoa vikwazo vya fedha dhidi ya serikali ya Palestina.