1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani na India zaafikiana kuhusu Nuklia

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5M

Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani na India wamefanikisha kile walichokiita kuwa hatua kubwa katika kutatua tofauti zao juu ya makubaliano ya kihistoria kuhusu suala la Nuklia.

Waziri wa mambo ya nje wa India Shivshankar Menon na mwenzake wa Marekani Condoleza Rice walikuwa na mazungumzo hapo jana kuhusu upinzani wa Marekani juu ya utekelezwaji wa makubaliano hayo ambayo yataipa India uwezo wa kupata technologia ya Kinuklia kwa ajili ya matumizi ya kiraia.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa mwaka jana ni muhimu kwa serikali ya mjini Delhi katika kupata Nishati bila ya nchi hiyo kusimamisha mpango wake wa Kinuklia kwa ajili ya matumizi ya kijeshi.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Nicholas Burns aliyongoza mazungumzo hayo anatarajiwa kwenda India baadae mwezi huu kukamilisha mpango huo.