1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani wawarudisha makwao watu sita kutoka Guantanamobay Cuba

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpx

Marekani imewarudisha makwao watu sita waliokuwa wakizuiliwa kama washukiwa wa ugaidi katika jela ya Guantanamo Bay Cuba.

Wizara ya mambo ya ulinzi ya Marekani imesema wawili miongoni mwa watu hao walirudishwa Tunisi na wengine wanne nchini Yemen.

Makundi ya kutetea haki za raia yamekosoa uamuzi wa kumrudisha mmoja kati ya washukiwa hao nchini Tunisia.

Kundi linalohusika na masuala ya haki za kikatiba limesema Abdullah bin Omar anakabiliwa na kitisho cha kupata mateso makubwa akirejeshwa nchini Tunisia.

Kiasi cha watu 375 bado wanazuiliwa Guantanamobay kwa tuhuma za kuhusiana na ugaidi.