1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani yaandaa vikwazo vipya dhidi ya Iran

19 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOY

Marekani inaandaa vikwazo vipya dhidi ya Iran siku kadhaa kabla mkutano wa viongozi unaopanga kujadilia mpango wa nuklia wa nchi hiyo unaozua utata.Kikao hicho kinapangwa kufanyika siku ya Ijumaa mjini Washington na kuandaliwa na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani chini ya usimamizi wa mwanadiplomasia wa ngazi za juu Nicholas Burns.Mawaziri wa mambo ya kigeni wanatarjiwa kuhudhuria kikao hicho.Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani Sean McComarck mkutano huo unalenga kupata suluhu ya utata wa mpango wenyewe wa Iran.Kiongozi huyo aliongeza kuwa Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleeza Rice anatarjiwa kukutana na wenzake watakaohudhuria mkutano huo mjini Newyork mwishoni mwa mwezi Novemba.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limeidhinisha maazimio matatu ya kuiwekea Iran vikwazo.Maazimio mawili yaliyipitishwa kwasababu ya taifa hilo kukataa kusitisha mpango wake wa kurutubisha madini ya uranium ambao Marekani inashuku huenda ukatumiwa kutengeza silaha za nuklia.Iran inashikilia kuwa mpango wake wa nuklia ni wa kutenegza nishati ya matumzi kwa raia wake.