1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani yaonywa juu ya kukiuka haki za binadamu

18 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9A

Wabunge kadhaa wa Umoja wa Ulaya wameionya Marekani dhini ya kukiuka haki za binadamu katika kampeni yake ya kupambana na ugaidi. Wabunge hao wamesema ukiukaji wa haki za binadamu utaathiri msimamo wa watu duniani juu ya kampeni hiyo.

Mbunge wa Uingereza bwana Evans amesema hayo kwenye kikao cha kamati ya baraza la wawakilishi mjini Washington.

Mbunge huyo pia amesema kuwa hadhi ya Marekani imezama kutokana na jela za siri za shirika lake la upelelezi CIA.