1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington:Marekani yasema itaitambua Kosovo ikiwa Urusi itaweka kikwazo

20 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgp

Marekani imetishia kuitambua Kosovo kama nchi huru kutoka Serbia, ikiwa Urusi itatumia kura yake ya turufu katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa, kukwamisha mpango ulioandaliwa na mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Marti Ahtisaari.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleeza Rice amesema uhuru utakua na uamuzi utakaochukuliwa kwa njia moja au nyengine.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov anaizuru Berlin leo kwa mazungumzo kuhusu swala la Kosovo. Waziri mdogo wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Gernot Erler amezitaka Serbia na Kosovo , jimbo ambalo wakaazi wake wengi ni wenye asili ya Albania, kutumaia muda uliosogezwa wa siku 120 zaidi, ili kufikia maridhiano juu ya kile kilichofafanuliwa katika muswada ulioandaliwa na Umoja wa mataifa. Serbia inapinga uhuru kwa jimbo hilo lenye wakaazi milioni mbili likiwa na jamii ndogo ya Waserbia Tangu 1999 linasimamiwa na umoja wa mataifa, baada ya majeshi ya shirika la kujihami la magharibi NATO yalipoyatoa kwa nguvu majeshi ya Serbia yalioingia Kosovo kuwaandama wenye asili ya kialbania.