1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Marekani yatoa mwito wa kupuuzwa vitisho vya Korea ya Kaskazini.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCz9

Marekani imepuuzia onyo la Korea ya Kaskazini ililolitoa kwa Korea ya Kusini ikiwa itatekeleza vikwazo ilivyowekewa Pyongyang.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bibi Condoleezza Rice ameitaka Korea ya Kusini kuonyesha wajibu wake kwa vikwazo vya kimataifa vilivyowekwa dhidi ya Korea ya Kaskazini kufuatia jaribio lake la bomu la nyuklia.

Bibi Rice ametaka jibu kali litolewe kutokana na ushupavu wa Korea ya Kaskazini litakaloambatana na azimio la Umoja wa Mataifa linalopiga marufuku kuuziwa zana za kijeshi na vitu vya anasa kwa Korea ya Kaskazini.

Hapo jana Korea ya Kaskazini imesema kwamba, hatua yoyote ya Soel katika kutekeleza vikwazo, inaweza kujikuta katika matatizo makubwa.