1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Matokeo ya uchaguzi yampa kiwewe rais Bush

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCux

Matokeo ya uchaguzi muhimu nchini Marekani yameanza kutolewa. Wananchi wa Marekani walipiga kura hapo jana katika uchaguzi wa bunge na baraza la seneti.

Chama cha Demokratic tayari kinaelekea kupata ushindi wa kiti cha seneti katika jimbo muhimu la Virginia .huku Keith Ellison wa chama cha Demokratic akipata ushindi wa kuwa muislamu wa kwanza kuingia bunge baada ya kuchaguliwa seneti wa jimbo la Minnesota.

Taarifa zinasema Chama cha Demokratic kimejipatia ushindi katika baraza la wawakilishi ushindi ambao umempa kiwewe na masikitiko rais Bush wa Republican.

Kiasi cha wamarekani millioni 200 walikuwa na haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa jumanne.