1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mzozo wa Iraq utahitaji maamuzi mazito aonya rais Bush

21 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChV

Rais Gorge Bush wa Marekani ameonya mzozo nchini Iraq utahitaji maamuzi magumu na kujitolea zaidi mwaka ujao.

Hivyo basi anafikiria kupeleka kwa muda mfupi jeshi zaidi katika nchi hiyo inayokabiliwa na mzozo.Akitoa hotuba yake ya mwisho wa mwaka kiongozi huyo wa Marekani alikiri kwamba hali nchini Iraq sio ya kuridhisha na kwamba waasi nchini humo wanavuruga juhudi za Marekani za kuweka usalama.Rais Bush anatarajiwa kutangaza mkakati wake mpya juu ya Iraq mnamo mwezi Januari.Wakati huo huo waziri wake wa Ulinzi Robert Gates ambaye alikutana na makamanda wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq amesema hawezi kutoa uamuzi juu ya hatua ya kuongeza wanajeshi nchini humo hadi atapokamilisha mazungumzo yake na pande zote husika.