1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush aamini kuwa Marekani itafanikiwa Iraq

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjO

Rais wa Marekani George W Bush anaamini kuwa nchi yake inaweza kufanikiwa katika vita dhidi ya Iraq.Hii ni kinyume na ripoti ya Ikulu ya Whitehouse.Ripoti hiyo inalenga kutoa ufafanuzi kuhusu malengo ya klijeshi na kisiasa ya Marekani tangu uvamizi ulipoanza.

Bunge la Marekani liliagiza hatua hiyo kuchukuliwa ili kutathmini mikakati mipya ya Rais Bush ya kuongeza idadi ya majeshi nchini Iraq.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo bado inasubiriwa baadhi ya malengo yamefikiwa hususan katika usalama ambapo idadi ya vifo vilivyo na misingi ya ghasia za kidini imepungua vilevile mashambulizi ya mabomu.

Hata hivyo ripoti hiyo haitaeleza kuwa uvamizi nchini Iraq haukufaulu.Rais Bush kwa upande wake anashikilia kuwa sharti muda uongezwe ili kujua hali halisi

''Ndio mwanzo tumeanza….hapa Washington baadhi ya watu wanapinga na kusema tuache.Naamini kuwa ni muhimu kwa taifa hili kumpa kamanda huyo mpya nafasi kutekeleza majukumu aliyopewa ndipo bunge litathmini hali halisi kabla kutoa uamuzi wowote.''

Wapinzani wa vita hivyo dhidi ya Iraq katika Bunge la Marekani wanasisitiza kuwa hakuna hatua zozote zilizopigwa tangu majeshi alfu 3 zaidi yalipopelekwa mapema mwaka huu.Nancy Pelosi ni spika wa bunge la Marekani ana mtazamo tofauti

''Wanataka vita hivi viishe.Wanataka majeshi yarudi nyumbani.Wanajua kwamba sera tulizofuata nchini Iraq tangu mwanzo hazijafanikiwa.''