1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush aupinga mswaada wa Congress kwa kura ya Turufu

2 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5K

Rais Gorge Bush ametumia kura yake ya turufu kuupinga mswaada wa kugharamia shughuli za wanajeshi wake nchini Iraq mswaada ambao unataka wanajeshi hao waanze kuondoka nchini humo kufikia tarehe mosi mwezi Oktoba.

Rais Bush amewaambia wamarekani kwamba kuweka ratiba maalum ya kuondoka Iraq kutasababisha hali ngumu kwa wanajeshi wake nchini humo.Ameongeza kusema kwamba ratiba hiyo itatoa sura mbaya kwa wairaq na magaidi.

Akikosoa hatua hiyo ya rais spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi amesema hawatamruhusu rais kuendelea na vita nchini Iraq.