1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Rais Bush kutangaza mpango wake wa Iraq

10 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCby

Rais George Bush wa Marekani anatarajiwa kutangaza mpango mpya hii leo kuhusu hatua ya kuongeza idadi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq.hatua hiyo inapingwa vikali na chama cha Democratik katika bunge la Congress.Kulingana na maafisa wawili wa serikali waliokataa kujitambulisha kiongozi huyo aidha anapanga kutoa mpango mzima wa Iraq utakaowapa mamlaka ya kuongoza nchi yao ifikapo mwezi Novemba.

Rais Bush anasubiriwa kutangaza kuwa anaongeza majeshi alfu 20 kujiunga na kikosi cha majeshi laki moja thelathini yaliyoko Iraq. Kiongozi huyo anakataa kuondoa majeshi yake nchini humo mpaka sasa.Wanachama wa Democratik wanaopinga hoja hiyo wanataka kuhusisha zaidi bunge la Congress katika maauzi ya kijeshi.

Wanachama wa Demokratik kinachosimamia maswala ya Bunge la Congress la Marekani wanapanga kupiga kura kuhusu mpango huo itakayowalazimu wanachama wa Republican wa chama cha Rais Bush kunukuliwa iwapo wanaunga mkono mpango huo mpya kuhusu Iraq.

Bunge la Congress halina uwezo wa kuamua idadi ya vikosi vinavyopelekwa Iraq kwani kulingana na katiba ya Marekani Rais ndiye Amri jeshi mkuu.