1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Uturuki kuimarisha majeshi yake mpakani na Irak

6 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79Y

Uturuki itaendelea kuimarisha majeshi yake kwenye mpaka wake na Irak ya Kaskazini licha ya lawama zinazotolewa na jumuiya ya kimataifa.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema hayo katika ziara yake nchini Marekani na kuongeza kusema kuwa uwezekano mkubwa upo wa kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya waasi wa Kikurdi.

Bwana Erdogan pia amekaribisha msimamo wa Marekani wa kuiunga mkono nchi yake katika kupambana na waasi wa Kikurdi wa chama cha PKK.

Rais Bush amemuhakikishia waziri mkuu wa Uturuki kwamba Marekani itashirikiana na Ankara kuhusu taarifa za kijasusi.

Rais Bush amependekeza kuwepo ushirikiano wa karibu wa kijeshi kati ya Marekani, Uturuki na Irak, huku akikitaja chama cha PKK kuwa ni adui wa mataifa hayo matatu.