1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.Vikwazo dhidi ya Sudan vyaimarishwa.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwi

Rais wa Marekani George W. Bush ameimarisha vikwazo vya kiuchumi vya Marekani dhidi ya Sudan ili kuilazimisha nchi hiyo kusitisha mauaji katika jimbo la Darfur, jimbo lililokumbwa na vita magharibi ya nchi hiyo.

Hatua hiyo inalenga dhidi ya makampuni yanayoendeshwa na serikali katika sekta ya mafuta nchini Sudan, pamoja na watu watatu, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa serikali.

Bush amesema kuwa Marekani pia itahimiza kupatikana kwa azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa litakaloihusu Darfur.

Lakini katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kutoa muda zaidi ili kuishawishi serikali ya Sudan iweze kuruhusu upelekaji wa jeshi la pamoja la kulinda amani kati ya umoja wa Afrika na umoja wa mataifa katika jimbo hilo.

Umoja wa mataifa unakadiria kuwa katika muda wa zaidi ya miaka minne kiasi cha watu laki mbili wameuwawa katika jimbo la Darfur na zaidi ya watu milioni mbili wengine wamelazimika kukimbia makaazi yao.