1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON.Wadau wa amani ya mashariki ya kati wakutana

2 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVl

Wawakilishi wa umoja wa mataifa , Marekani, Urusi na wa umoja wa ulaya leo wamakutana mjini Washington, Marekani katika juhudi za kuufufua mchakato wa kuleta amani katika mashariki ya kati.

Lengo la mkutano huo ni kuutia msukumo mpya mchakato huo wa kuleta amani baada ya kuzorota kwa muda wa miezi kadhaa.

Mkutano huo unafuatia mazungumzo yaliyofanywa na kansela wa Ujerumani bibi Angela Merkel na waziri wa mambo ya nje wa Marekani bibi Condoleeza Rice.

Wadau wa amani ya mashariki ya kati awali hawakufikia maelewano kuhusu iwapo kundi la nchi za magharibi ziendelee kuzuia misaada kwa serikali ya Hamas inayotawala maeneo ya Palestina.

Urusi ilipendekeza mapema wiki hii kuwa vikwazo dhidi ya serikali ya Hamas viondolewe.

Nchi za kiarabu hususan Misri zinataka wadau hao kuzilazimisha Israel na Palestina zifikie maamuzi kuhusu hali ya mipaka ya Jerusalem na wakimbizi wa ukingo wa magharibi.