1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Wolfowitz akana kukiuka sheria za maadili

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1d

Kiongozi wa Benki ya Dunia Paul Wolfowitz anakana kukiuka maadili baada ya kumwongeza mshahara mpenzi wake Bi Shaha Riza aliye pia mfanyikazi wa benki hiyo.

Bodi ya Benki ya Dunia inajadilia uwezekano wa kumruhusu Bwana Wolfowitz kuendelea na wadhifa wake jambo linalopingwa vikali na serikali za Ulaya.Rais wa Marekani George W Bush anamuunga mkono kiongozi wa benki hiyo aliyehusika kwa karibu na mpango wa uvamizi wa Iraq mwaka 2005.Marekani kwa kawaida huteua kiongozi wa Benki ya Dunia.

Hata hivyo Marekani huenda ikabadili msimamo wake kwa kumaliza kesi hiyo ya kukiuka maadili bila kumlazimisha Bwana Wolfowitz kujiuzulu.Badala yake Bodi ya Benki huenda ikatathmini uwezo wa Paul Wolfowitz wa kuongoza Shirika hilo lililo na nchi 185 wanachama kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Whitehouse Tony Snow.

Bi Shaha Riza mpenzi wake Bwana Wolfowitz aliongezwa mshahara na kupandishwa cheo miezi mitatu baada ya Bwana Wolfowitz kushika wadhifa huo mwezi Juni mwaka 2005.

Paul Wolfowitz aliye na umri wa miaka 63 anasisitiza kuwa alifuata mapendekezo ya kamati ya maadili ya Benki ya Dunia na kulaumu maadui wake wanaoendesha kampeni ya kumwondoa.