1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Wolfowitz asema "siondoki"

16 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9T

Rais wa benki ya dunia bwana Paul Wolfowitz amesema hana mpango wa kujiuzulu licha ya kashfa inayomkabili.

Bwana Wolfowitz amesema hayo alipozungumza na waandishi habari ambapo alieleza kuwa anakusudia kuendelea na kazi yake.

Rais huyo wa benki ya dunia yupo chini ya shinikizo kubwa akitakiwa ajiuzulu baada ya kukiri kwamba alimsaidia mfanyakazi mwanamke aliekuwa karibu naye sana ,kupandishwa cheo na kuongezwa mshahara.