1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washinton. Mwanajeshi afungwa kwa kuhusika na kifo cha raia.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD59

Daktari wa kikosi cha majini cha jeshi la Marekani amehukumiwa kwenda jela kwa kuhusika katika kifo cha raia mmoja wa Iraq mapema mwaka huu.

Jaji wa mahakama ya kijeshi amemhukumu Melson Bacos kwenda jela miaka 10 lakini ikapunguzwa hadi mwaka mmoja katika makubaliano baada ya kuomba.

Hii imekuja baada ya Bacos kutoa ushahidi dhidi ya wanajeshi wengine saba ambao wanashitakiwa kwa mauaji ya mtu mmoja mwenye umri wa miaka 52 Hashim Ibrahim Awad karibu na mji wa Baghdad.

Bacos aliiambia mahakama katika kituo cha kijeshi cha Marekani cha Camp Pendleton , Califonia kuwa alijisikia mgonjwa hadi katika matumbo, baada ya Awad kuburuzwa kutoka nyumbani kwake na kupigwa risasi kinyama. Amesema kuwa wamemuua Awad kutokana na hasira baada ya kushindwa kumpata mtu aliyekuwa akishukiwa kuwa ni mpiganaji.