1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINTONG: Bush asema Marekani haina mpango wa kuishambulia Iran

13 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSa

Rais George W Bush wa Marekani amesema tetesi kwamba Marekani inapania kuivamia kijeshi Iran ni porojo zisizo na msingi wowote.

´Nabashiri hisia zangu kwa kelele zote ujuazo kwamba anataka kwenda vitani. Kwanza kabisa sielewi mbinu zake na nadhani ningesema ni za kisiasa.´

Hata hivyo rais Bush amesema anatumai kwamba wabunge wa upinzani katika bunge la Congress wataelewa vipi Irani inavyoweza kuwa hatari iwapo itamiliki silaha za kinyuklia. Rais Bush anataka kuwepo sera thabiti zikazoweza kuzuia matatizo yanayoweza kusababishwa na mpango wa nyuklia wa Iran.