1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Washirika wa Imran Khan waongoza uchaguzi Pakistan

Iddi Ssessanga
9 Februari 2024

Wagombea watiifu kwa waziri mkuu wa zamani wa Pakistan aliyeko gerezani, Imran Khan, wameshinda viti vingi mpaka sasa, wakiwa mbele ya vyama viwili vikongwe vinavyoaminika kupendelewa na jeshi.

https://p.dw.com/p/4cEVU
Bango la wagombea uchaguzi wa chama cha Nawaz Sharif.
Bango la wagombea uchaguzi wa chama cha Nawaz Sharif.Picha: Aamir Qureshi/AFP

Khan alizuiwa kushiriki uchaguzi wa Alhamis (Februari 8) na chama chake cha Pakistan Tahreek-e-Insaf ( PTI) kilizuwiwa kufanya mikutano ya kampeni na kuondolewa kwenye karatasi za kura, na hivyo kuwalazimu wanachama wake kushiriki kama wagombea huru.

Soma zaidi: Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo

Lakini matokeo ya awali yanaonesha wafuasi wa PTI mpaka sasa wameshinda karibu vita 49 katika bunge la taifa lenye jumla ya vitia 266, dhidi ya viti 42 vya chama cha Pakistan Muslim League- Nawaz (PML-N) na kile cha Pakistan Peoples Party (PPP) baada ya zaidi ya nusu ya majimbo kukamilisha hesabu.