1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa 2 wakamatwa kuhusu mauaji ya Bhutto

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cuzx

ISLAMABAD: Wizara ya Mambo ya Ndani ya Pakistan imethibitisha kuwa washukiwa 2 wamekamatwa kuhusika na mauaji ya waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto yaliyotokea Desemba mwaka jana.Kwa mujibu wa waziri wa ndani Syed Kamal Shah,siku ya Ijumaa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 na mshirika mwenzake walikamatwa kaskazini-magharibi ya nchi.

Ripoti zinasema kuwa washukiwa hao 2 ni wafuasi wa kiongozi wa kikabila,Baitullah Mehsud katika eneo la kaskazini-magharibi linalopakana na Afghanistan.Serikali ya Pakistan inamlaumu Baitulla Mehsud kwa mauaji ya Benzair Bhutto aliekuwa kiongozi wa chama cha upinzani cha PPP.