1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa ugaidi 14 watiwa mbaroni Hispania

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cupi

MADRID: Polisi nchini Hispania hii leo imewakamata watu 14 wanaoshukiwa kuhusika na ugaidi.Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hispania,Wapakistani 12 na Wahindi 2 walikamatwa mjini Barcelona kaskazini mwa nchi katika msako uliopangwa pamoja na Kituo cha Upelelezi cha Hispania.

Wakati huo huo serikali haikupinga uwezekano wa kuwatia mbaroni washukiwa zaidi.Waziri Mkuu wa Hispania Luis Rodriguez Zapatero amethibitisha ripoti hiyo na kuongezea kuwa uchunguzi ungali ukiendelea.