1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasichana Kenya watumia miili yao kujikimu kimaisha

25 Novemba 2014

Wasichana wadogo nchini Kenya wamekuwa wakilazimika kujiingiza katika unywaji pombe na uuzaji wa miili yao kama njia ya kujipatia chakula wao na familia zao.

https://p.dw.com/p/1Dtbf
Sextourismus Prostitution Kenia
Picha: TONY KARUMBA/AFP/Getty Images

Brittanie Richardson binti wa kimarekani mwenye umri wa miaka 27 ameanzisha kampeni ya kupinga hali hiyo baada ya ziara yake iliyoshuhudia vitendo hivyo vya mara kwa mara kwa familia zilizo na hali ngumu ya maisha.

Mjini Nairobi kuna msongamano mkubwa wa makazi duni, watoto wenye njaa mara nyingi wanafanya biashara ya miili yao ili kujipatia pesa kidogo au chakula, mji huo wenye wakazi milioni 3.1, ni nyumbani kwa watu milioni 2 wanaoishi katika makazi duni na idadi ya watu katika makazi duni katika mji huo mkuu wa Kenya inakua kwa asilimia 6 kwa mwaka.

Kulingana na shirika la kuwahudumia watoto la umoja wa Mataifa Kenya ina watoto wanaofanya kazi ya ngono 30,000 waliogawanyika katika pembe zote za fukwe za utalii, huku ukahaba miongoni mwa watoto likitambuliwa kama tatizo linalohitaji kukabiliwa kwa utekelezaji wa sheria kali na kuwapa wasichana hao ncji mbadala ya kujikwamua kutokana na mtego huo.

Sextourismus Prostitution Kenia
Eneo la fukwe za utalii nchini KenyaPicha: Getty Images

Richardson kutoka mji wa Atlanta, katika jimbo la Georgia nchini Marekani hakuwa na wazo juu ya kiwango cha tatizo nchini Kenya mpaka pale aliponza kusafiri mara kwa mara Afrika wakati akiwa chuoni. Awali alikuwa akisaidia nchi ya Afrika Kusini kupambana na kukosekana haki ya kijamii na kisha nchini Msumbiji.

Mkutano na mwanamke wa Canada nchini Msumbiji ambaye alihitaji msaada wa kuanzisha makaazi ya kuwaokoa watoto walionasa katika ukahaba, ulimfanya Richardson kuelekea katika mji wa Mtwapa nchini Kenya, ambao umekuwa na sifa mbaya ya ukahaba katika eneo la pwani.

Richardson alisema, na hapa ninamunukuu, "Ulikuwa ni wakati wa kuhuzunisha na kushitusha kuona binti wa miaka 15 kiasi kidogo mwenye miaka minane akiinieleza kuwa analazimika kufanya ngono ili aweze kupata chakula kiukweli nilishituka.

Richardson alijiona yeye mwenyewe nakuwa mmoja wa watu wanaongoza harakati za kuendesha kampeni ya ngazi za chini kupambana na umasikini kuacha kuwapeleka watoto wanaotoka katika makazi duni katika biashara ya ngono.

Lakini baada ya miaka miwili ya harakati za kituo cha Mtwapa, Richardson anataka kufanya kazi zaidi ya kusaidia na mwezi wa nne mwaka huu aliweka kitengo cha sanaa na kukomesha unyanyasaji chenye lengo la kusaidia watumwa wa ngono kupitia kufanya sanaa ambayo anaona itakuwa tiba na dawa.

Kenya Airways Flughafen Nairobi ARCHIV
Uwanja wa ndege wa Kimataifa KenyaPicha: picture-alliance/dpa

Kwa kusaidiwa na mfanyakazi wa kijamii, Richardson aliwachagua wasichana 10 wenye umri kati ya miaka minane na 16 waliokuwa wakiishi katika makazi duni ya Sinai kuwa sehemu ya mpango wake. Sinai ni moja ya makazi 200 duni mjini humo.

Richardson alisema Kati ya wasichana hao 10 kati yao ama wamebakwa au wamelazimishwa na umasikini au wazazi wao kufanya ngono ili kujipatia fedha Aliongeza kuwa majukumu yake katika kazi hiyo inatokana na uzoefu wake kutokana na kufanyiwa unyanyasaji wa kingono wakati wa utoto wake na ndugu wa karibu katika familia yake lakini kila mtu amejaribu kupuuza jambo hilo.

Anaipongeza asasi ya vijana ya michezo ya kuigiza ya Freddie Hendricks ya mjini Atlanta, iliyoanzishwa na mwanamuziki wa muziki wa miondoko ya jazz kwa kuyaokoa maisha yake. Alisema aliona upendo wa kweli waliomuonyesha kama mwathirika na anataka kufanya vivyo hivyo kwa wasichana wengi.

Lakini kazi yake itafanikiwa kwa gharama na Richardson ameweza kufanikisha uungwaji mkono kutoka idadi kubwa ya wasanii, wanaharakati mjini New York ambao wamekuwa wakiendesha jitihada za kuchangisha kwa ajili ya onyesho lenye kupinga na kukemea vitendo vya unyanyasaji wa ngono dhidi ya wasichana.

Mwandishi: Nyamiti Kayora/RTRE

Mhariri: Josephat Charo