1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasimamizi wa Nchi za Magharibi hawakualikwa Zimbabwe

8 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DKzc

HARARE:

Serikali ya Zimbabwe imesema,haitowaruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za magharibi kusimamia uchaguzi mkuu utakaofanywa nchini humo Machi 29.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Zimbabwe,Urusi na baadhi ya nchi zisizopendelea upande wo wote ndio zilizoalikwa.Wajumbe kutoka mkoloni wa zamani Uingereza,Umoja wa Ulaya na Marekani wamepigwa marufuku. Badala yake serikali ya Zimbabwe inataka wajumbe kutoka nchi za Umoja wa Afrika kusimamia uchaguzi huo.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anatuhumiwa na nchi za magharibi kukiuka haki za binadamu na kudharau misingi ya demokrasia.