1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi kuhusu matangazo ya matokeo ya kura waibuka

1 Novemba 2010

Tanzania katika mtihani wa matokeo baada ya uchaguzi wa jana (31 Oktoba 2010) kwenda kwa amani. Ripoti na mahojiano mbalimbali kutoka huko yanaonesha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi

https://p.dw.com/p/PvOc
Bendera za vyama vitatu vikubwa nchi Tanzania. Kutoka kushoto CCM, CUF na CHADEMA
Bendera za vyama vitatu vikubwa nchi Tanzania. Kutoka kushoto CCM, CUF na CHADEMAPicha: DW

Baada ya hapo jana (31 Oktoba 2010) kuripotiwa kwamba zoezi la upigaji kura lilikwenda vizuri katika pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Bara na Zanzibar, taarifa za leo (1 Novemba 2010) ambapo matokeo yalitarajiwa kuanza kutoka imebadilika kidogo. Kuna wasiwasi wa kutibuka kwa hali ya usalama na amani uliozoeleka nchini humo, taifa ambalo linachukuliwa kuwa mfano Barani Afrika kwa utulivu.

Hapa tunawaletea taarifa mbalimbali za waandishi wetu walioko sehemu tafauti nchini Tanzania pamoja na mahojiano kati ya Deutsche Welle na wahusika mbali mbali wa uchaguzi huu wa nne wa vyama vingi katika nchi hii ya Afrika Mashariki