1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasiwasi wa Malawi kuhusu makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi

Jane nyingi27 Agosti 2007

Wenye viwanda, wafanyibiashara na hata maafisa wa serikali nchini malawi wanawasiwasi wa kuingia kwa mwaka ujao.Tarehe mosi januari mwakani ndio siku ambayo makubabiliano ya ushirikiano wa kiuchumi yanayojadiliwa kati ya umoja wa ulaya na kundi la mataifa sita kutoka Africa, Caribbean na Pacific yatakapoanza kufanya kazi.

https://p.dw.com/p/CHjY
malawi
malawi

Serikali ya malawi kwa muda mrefu imekuwa ikiwashawishi wananchi wa taifa hilo maskini kusini mwa africa kuwa makubaliano hayo yananuia kuwanufaisha.Chini ya makubaliano hayo serikali inasema itaweza kupata usadizi kutoka jumuiya ya ulaya ili kuboresha miundo msingi hasa katika secta ya uchukuzi na nishati.Hata hivyo kunao wanaohisi kuwa huenda makubaliano hayo ya ushirikiano wa kiuchumi yakawa balaa .Mapema mwaka huu wizara ya biashara nchini Malawi ilieleza kutoridhishwa kwake na njisi mashirika yasiyoyakiserikali yenye ushawishi mkubwa nchini humo yameendelea kuyapinga makubaliano hayo.

Hata walimwandikia barua mwezi aprili rais wa umoja wa ulaya Chancellor wa ujerumani Angela Merkel kuwa makubaliano hayo yanayopendekezwa yakaenda kinyume na maslahi ya malawi na mataifa mengine maskini 15 yaliyoko katika jumuiya ya kiuchumi ya mashariki na kusini mwa Africa-Comesa,kwa kuwa yanawazuia kuvilinda viwanda vyao kutokana na ushuru wa forodha na maswala mengine.

Kwa sasa serikali inaonekana kubadili msimamo wake wa awali na kujiunga na mashirika yalisiyo yakiserikali.Wiki iliyopita wizara ya biashara ilifanya mkutano na wenye wiwanda na wafanyibiasahra nchini Malawi kuibuka na orodha ya bidhaa za kutoka viwanda vyao ambavyo huenda vikadhuriwa na ushindani huo wa kimataifa.

Katika Mkutano huo wadau waliafikia kuwa chini ya makubaliano hayo sheria zilivyo kwasasa ,zinalizuia taifa la malawi kupenya katika soko la umoja wa ulaya.

Zaidi ya makampuni 40 ziliwakilishwa kwenye mkutano huo na pamoja na serikali waliafikia kuwa bidhaa 102 zinahitajika kulindwa.Baadhi ya bidhaa hizo ni zile zinazoipa Malawi pato la kigeni ambazo ni pamoja na tobacco,majani chai,pamba sukari na bidhaa zinazotokana sukari.

Orodha hiyo ilitengezwa kulingana na vigezo mbalimbali. Kwanza pato la kigeni linalotokana na bidhaa hizo na pili uwezo wa viwanda hivyo kuwapa ajira wamalawi wengi.

La tatu ni kuvilinda viwanga changa,ikiimarisha viwanda vipaya au vile vinavyochipuka ambayo vinamatatizo ya kujiimarisha kutoka na ushindani mkali kutoka kwa viwanda vilivyo katika mataifa ya kaskazini.

Mataifa mengi yaliyostawi yaliyoko katika jumuiya ya ulaya viwanda vya nguo na chuma hutoa ajira kwa watu wengi katika mataifa hayo na hivyo kurodheshwa kati ya vile vinavyohitajika kulindwa. Iwapo viwanda hivyo vingefungwa watu wengi wagepoteza njia ya kujipatia pato.

Malawi lazima ingetoa orodha hiyo na kuiwasilisha katika afisi kuu za jumuiya ya kiuchumi ya mashiriki na kusini mwa africa-Comesa kufikia Agosti 15 mwaka huu. Jumuiya hiyo inakusanya orodha ya bidhaa kutoka mataifa wanachama zinazohitajika kuzunguziwa wakati wa mkutano wa makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi ili kuweza kupewa ulinzi.

Bidhaa elfu2,900 zimeorodheshwa kutoka mataifa ya mashariki na kusini mwa africa huku Ugnda na Kenya ikiwa na orodha ya bidhaa nyingi.

Baada ya mkutano wa 12 wa mataifa hayo uliandaliwa na afisi kuu za comesa mwanzo wa mwezi huu, mataifa husika yaliombwa kupunguza orodha ya bidhaa wanazosema vinahitajika kulindwa baada ya kufanya mkutano wa wadau.

Mkutano huo ulipendekeza mataifa hayo kuondoa bidhaa za matibabu,dawa, na vifaa vya mafunzo amabayo havitozwi ushuru.