1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataliani kufanya uchaguzi Jumapili

23 Februari 2013

Wagombea katika uchaguzi mkuu wa Italia wamefanya kampeni zao za mwisho Ijumaa (22.02.2013) kabla ya uchaguzi muhimu. Wawekezaji wa kimataifa wameonya kuwa matokeo yasiyokuwa wazi huenda yakatikisa uchumi wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/17kUx
Italy's Democratic Party (PD) leader Pier Luigi Bersani gestures as talks during a political rally in downtown Milan February 17, 2013. Voters will go to the polls in a parliamentary election on February 24 and 25. REUTERS/Alessandro Garofalo (ITALY - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Kiongozi wa chama cha PD Pierluigi BersaniPicha: Reuters

Wataliani watapiga kura kesho Jumapili (24.02.2013) na Jumatatu (25.02.2013) wakati wakiendelea kukabiliana na kipindi kirefu cha mdororo wa uchumi katika muda wa miongo miwili pamoja na serikali kubana matumizi hali ambayo imesababisha malalamiko makubwa katika taifa hilo lenye uchumi wa tatu kwa ukubwa katika eneo la euro.

Matokeo ambayo yanatarajiwa ni serikali itakayoongozwa na vyama vya mrengo wa kati kushoto utakaoongozwa na kiongozi wa chama cha Democratic Pier Luigi Bersani, zamani akiwa mfuasi wa ukomunist ,mwenye tabia ya kujiamini na ambaye hivi sasa anakumbatia kwa kiasi kikubwa mawazo ya uchumi unaopendelea masoko.

Former Italian Prime Minister Silvio Berlusconi gestures during a political rally in Turin February 17, 2013. REUTERS/Giorgio Perottino (ITALY - Tags: POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY)
Waziri mkuu wa zamani Silvio BerlusconiPicha: Reuters

"Nina imani kabisa kuwa nitashinda," Bersani amesema katika moja kati ya mahojiano yake kabla ya Jumamosi, ambapo wagombea hawaruhusiwi kufanya kampeni.

Masoko ya fedha yana shaka

Lakini matokeo bila shaka yanafahamika na iwapo Bersani ataunda muungano imara kwa kuwa na wingi katika mabaraza yote ya bunge ni jambo la kutia shaka sana, hali itakayoweka masoko ya fedha katika hali shaka shaka.

Waziri mkuu anayemaliza muda wake Mario Monti amekamilisha kampeni yake mjini Florence, akivishutumu vyama vya mrengo wa shoto kwa kuwa wafungwa wa nadharia yao isiyopindika na kumshutumu waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi kwa kuwavunjia adabu wanawake.

Berlusconi atoa ahadi

Ahadi ya Berlusconi katika barua ambayo ilionekana kuwa rasmi ya kuwarudishia fedha zao Wataliani zilizokatwa kutokana na kodi ya umiliki wa mali iliyowekwa na Monti ilisababisha baadhi ya watu kuweka misururu mirefu katika ofisi za posta wakidai fedha zao.

Miji kadha barani Ulaya itakuwa inatega sikio kwa karibu iwapo Italia ikirejea katika miaka ya matumizi holela ya fedha za umma inaweza kuzusha maafa kwa mataifa ya eneo la euro.

Five-Star Movement leader and comedian Beppe Grillo gestures during a rally in Turin February 16, 2013. REUTERS/Giorgio Perottino (ITALY - Tags: POLITICS ELECTIONS)
Mchekeshaji wa zamani Beppe GrilloPicha: Reuters

"Tunaamini kuwa hali ya kitisho ipo kwamba baada ya uchaguzi wa Februari 24-25 huenda kukawa na upotevu wa msukumo kuhusu mageuzi muhimu ya kuongeza kasi ya matumaini ya ukuaji wa uchumi wa Italia," shirika la upangaji wa viwango vya uwezo wa kukopa la Standard & Poor's limesema katika ripoti yake wiki hii.

Kundi la utafiti lenye makao yake makuu mjini London la Capital Economics limeonya kuwa, "bunge ambalo litashindwa kupatikana wingi kwa upande mmoja linaweza kuirejesha Italia na eneo la euro katika mzozo".

Vituo vya uchaguzi

Vituo vya uchaguzi vitafunguliwa mapema asubuhi kesho Jumapili na kufungwa saa moja jioni saa za Ulaya ya kati. Siku ya pili ya uchaguzi Jumatatu uchaguzi utaanza saa 12 asubuhi na kumalizika saa tisa mchana, baada ya hapo matokeo ya awali yatatangazwa baadaye jioni ya Jumatatu.

Italy's outgoing Prime Minister Mario Monti speaks during a meeting in Rome February 15, 2013. REUTERS/Tony Gentile ( ITALY - Tags: POLITICS BUSINESS)
Waziri mkuu anayeondoka madarakani Mario MontiPicha: Reuters

Mario Monti , profesa muumini wa kanisa Katoliki ambaye anamaliza muda wake wa uongozi , ni chagua la wazi la kanisa hilo mjini Vatican katika uchaguzi huo. Lakini kujiegemeza kwake na muungano wa kati kushoto kunalifanya kanisa hilo kusita kidogo. Kura za Wakatoliki si za kupuuza katika siasa za Italia, ni mchekeshaji Beppe Grillo pekee ambaye amelipinga hadharani kanisa na amekataa mawazo yao.

Mwandishi. Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Grace Patricia Kabogo