1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wataliban wasema wameua mateka wa Kijerumani

P.Martin21 Julai 2007

Ripoti zisizothibitishwa zimemnukulu msemaji wa Taliban akisema,mateka wote 2 wa Kijerumani waliokamatwa siku ya Jumatano katika Wilaya ya Wardak nchini Afghanistan wameuawa.

https://p.dw.com/p/CB2e
Wanamgambo wa Taliban wanataka majeshi ya kigeni yaondoke Afghanistan
Wanamgambo wa Taliban wanataka majeshi ya kigeni yaondoke AfghanistanPicha: AP

Yousuf Ahmad anaesemekana kuwa ni msemaji wa Taliban, aliviarifu vyombo vya habari kwa njia ya simu kuwa mateka hao wa Kijerumani waliuawa baada ya kumalizika ule muda uliotolewa,kuanzisha moja kwa moja majadiliano pamoja na serikali za Ujerumani na Afghanistan.

Wataliban wanataka Ujerumani iwaondoshe wanajeshi wake 3,000 ambao ni sehemu ya vikosi vya NATO vinavyosimamia usalama nchini Afghanistan.

Wahandisi hao wawili wa Kijerumani na wafanyakazi wenzao watano wa Kiafghanistan,walitekwa nyara walipokuwa wakifanya kazi katika mradi wa bwawa nchini Afghanistan.