1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watalii walionusurika warejea Ubeligiji

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cupc

BRUSSELS: Wabeligiji 2 walionusurika chupuchupu baada ya basi la watalii kushambuliwa nchini Yemen, wamerejea Ubeligiji.Maiti za watalii 2 wa kike waliouawa na watu waliofyatulia risasi basi la watalii zitarejeshwa Ubeligiji baadae.

Kundi la watalii lilishambuliwa,lilipokuwa njiani kwenda kuzuru mji wa Shibam wa karne ya 16.Mji huo wa kale umeorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa-UNESCO kama kituo cha urithi wa kitamaduni.