1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watawa wafanya maandamano Tibet.

27 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DVf2

Lhasa.

Kiasi cha watawa 24 wamefanya maandamano kwa muda mfupi mbele ya waandishi wa habari wa kigeni wanaotembelea mji mkuu wa Lhasa.

watawa hao walikuwa wakimshambulia kwa maneno afisa mmoja wa China ambaye alikuwa akiwapa taarifa waandishi wa habari, ambapo katika wakati fulani watawa hao waliishutumu serikali ya China kwa kudanganya kuhusiana na hali katika jimbo la Tibet.

Tukio hilo lilitokea wakati ziara iliyopangwa katika jimbo la Tibet kwa waandishi wa habari wa kigeni , ikiwa ni ya kwanza tangu ghasia kuzuka katika jimbo hilo mapema mwezi huu.

Hapo mapema, rais wa Marekani George W. Bush alieleza wasi wasi wake kuhusiana na mzozo huo.

Alimpigia simu rais mwenzake wa China Hu Jintao na kuitaka nchi hiyo kuanza mazungumzo na kiongozi wa kidini wa Tibet anayeishi uhamishoni.

China inamshutumu Dalai Lama kwa kuhusina na hali hiyo ya ghasia ambayo imesababisha watu kadha kuuwawa.

Ameshutumu maandamano hayo yaliyokuwa na ghasia , akitaka kuwe na mazungumzo na maafisa wa China.