1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto robo milioni wakabiliwa na utapiamlo Nigeria

10 Septemba 2016

Wakati Serikali ya Nigeria ikiendelea na uchunguzi wizi wa chakula cha misaada unadhaniwa kufanywa na baadhi ya maafisa, madaktari wasio na mipaka wanasema watoto karibu robo milion wameathiriwa na utapiamlo

https://p.dw.com/p/1Jzjn
Wananchi waliokimbia makazi yao wakiwa katika ya kambi MaiduguriPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Ola

Madaktari hao wanasema kunahitajika misaada zaidi kutoka nje ili kuweza kunusuru maisha ya watoto ambao wengi wao wako katika hali mbaya licha ya kuwa kuna watu wengine karibu milioni mbili nchini humo ambao hawajaweza kufikiwa kutokana na mazigira wanayoishi na hivyo kushindwa kufanya tathmini kufahamu wanahitaji msaaada kiasi gani

Katika kambi ambayo idadi ya waathirika imekuwa ikiongezeka licha ya eneo hilo kuendelea kuongezwa pia baadhi ya watoto wameathiriwa vibaya sana na njaa na kuelezwa kuwa wanaweza kufariki ndani ya saa 24

Wakimbizi zaidi ya milion moja wamehifadhiwa katika kambi hiyo mjini Maiduguri lakini nje tu ya kambi hizo kuna soko ambalo huuzwa bidhaa kama vile mananasi, machungwa, kabeji, nyanya na karots lakini wengi wa wakimbizi hawewezi kununua kutokana na kutokuwa na pesa za kutosha kujipatia mahitaji hayo muhimu kwa afya zao

Issiaka Abdou Kiongozi katika kitengo cha dharura cha madaktari wasio na mipaka anasema wanapokea watoto wenye utapiamlo wengi mara kwa mara kutoka katika makambi hali inayowaonyesha kuwa wanahitaji kufanya zaidi kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu hasa katika kipindi ambapo malaria na kuhara kumeongezeka

Watoto wengine ambao hawajafikiwa wako hatarini zaidi

Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kuna watoto wengine milioni moja ambao wako katika maeneo hatari zaidi kufikika kutoka na hofu ya kuvamiwa na kundi hilo, baada ya mwezi Julai kufayika sambulio la roketi kuwalenga watu kadhaa na wafanyakazi wa shirika hilo waliokuwa wakipeleka misaada ya chakula katika eneo la Bama ambako kulikuwa na watu sita waliokuwa katika hali mbaya zaidi ya utapiamlo pamoja na kuhara, katika tukio hilo watu watatu walijeruhiwa

Hungerprojekt Mangel4
Mtoto ambaye ameathirika na utapiamloPicha: dapd/DW

Mwezi huo huo wa Julai gari la madaktari wasio na mipaka pia ililipuliwa barabarani japo hakukuwa na mtu aliyejeruhiwa vibaya

Hassan Mohamed na watoto wake watano wanaotunzwa kituoni hapo, wameathiriwa na njaa pamoja na kuishi maisha ya wasiwasi tangu mume wake alipouwawa na magaidi hao wakati mtoto wake wa kwanza akiwa na miaka saba, akiwa kituoni hapo anajaribu kumyonyesha mtoto wake mwenye umri wa miezi 18 aliyedhoofika sana kiasi cha kushindwa kumeza chochote na kwa muda wote amekuwa akiishi kwa kupatiwa chakula kwa njia ya mrija kupitia katika pua. Hassana anasema wamekuwa wakikimbia kwa sasa lakini Boko haram hawajawahi kuwa mbali nao na kuongeza kuwa

Wanawake wamekuwa wakifariki wakati wa wakijifungua wakiwa porini na wengine wakiwa njian kukimbia kwenda maneo nawayoweza kupata chakula na wengine hukimbia kuokoa maisha na kuwacha watoto na hivyo watoto wengi waliachwa porini.

Licha ya kuendelea kuishi kama wakimbizi katika kambi hiyo, changamoto kubwa kwao sasa ni jínsi ya kupata chakula kwa ajili yao na watoto wao

Mwandishi: Celina Mwakabwale/AP

Mhariri:Yusuf Saumu