1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watoto wa mitaani wa Rwanda

Kitojo, Sekione28 Julai 2008

Watoto kadha nchini Rwanda huishi bila wazazi kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo watu kadha wamepoteza maisha yao.

https://p.dw.com/p/ElTl





Nchini Rwanda wanakua watoto wengi bila wazazi. Sababu yake kuu ni miaka kadha ya vita vya wenyewe nchini humo ambapo watu laki moja wamepoteza maisha yao katika miaka ya 90. Si watoto wote ni yatima , wengi wao wanaishi katika kile kinachoitwa nyumba za watoto. Wakipata misaada kutoka kwa ndugu, lakini wengine hujisaidia wenyewe.



Naamka, wakati kukipambazuka, na hii ni karibu saa 12 asubuhi. Baadaye nasafisha eneo hili na nyumba yetu. Baadaye nakwenda mjini kuuliza iwapo wanaweza kunipatia kazi ya kufanya, ama wanahitaji msaada kwa kazi za shamba. Kama nakubaliwa, naanza kazi saa moja asubuhi na kufanyakazi hadi mchana.



Rosine anapata kiasi cha Francs za Rwanda 400 kwa kazi za shamba ambapo anatumia jembe la mkono, hii ni karibu senti 50 za Euro. Kama hapati kazi anashughulika katika kishamba chake kidogo karibu na nyumba anakoishi, akiwa amepanda mtama pamoja na viazi vitamu.

Hatuna fedha ya kununua saa. Lakini saa ninayo kichwani mwangu. Napima kichani , kwamba hivi sasa jua liko hapa au pale na hivi sasa ni saa fulani, naweza kufahamu. Hivi sasa ni saa ngapi kwa wastani. Hadi sasa nimeweza kufanikisha kila kitu.

Mababu na wazee wetu hawana watoto tena, mashangazi wanaishi mbali sana, na kutoka kwa majirani hatutarajii mengi.



Majirani wako tu na hakuna cha zaidi. Pia hata kama jioni hatuna chakula, na wanafahamu hilo, hawatusaidii. Hakuna kitu kabisa, ambacho tunawategemea wao . Wanajiangalia wao tu. Watu wa siku hizi wako hivyo.



Iwapo hawana bahati kabisa kupata msaada wa kimataifa katika mpango wa mikopo, kama ilivyo kwa familia Rosine kutoka katika kile kinachoitwa mtandao wa msaada wa kiutu, inabidi wajisaidie wenyewe. Paul Tschembe, ni mchungaji wa kanisa la eneo la Mbazi.



Kwa upande wake serikali haiko katika hali ya kuwasaidia watoto yatima, kwasababu ni wengi mno. Pekee katika kanisa langu ziko familia 200 ambazo zina watoto yatima, na wengine hawajulikani. Hii kwa kweli ni changamoto kubwa. Sio rahisi , lakini tunashukuru, wengi wamebaki katika majumba yao, na wanajaribu kuishi kwa njia zao wenyewe. Hapa tuko karibu na mji wa Butare, wengine wanakwenda huko, na wanakuwa watoto wa mitaani.

Maisha hapa tayari ni magumu kwa familia za kawaida zikiwa na wazazi wote wawili, ni ngumu kiasi gani basi kuwa mtoto yatima.


Kuwa na chakula cha jioni ni lazima chakula hicho kipikwe mchana. Rosine na mtama wake huenda kwa jirani ambaye anajiwe la kusagia, ambapo anaweza kulitumia. Kwa jiwe hili anasaga unga kwa kutumia jiwe hili. Unga unasagwa hadi kuwa laini kabisa. Wakati huo anacheza mdogo wake karibu yake. Emanuel.



Baadhi ya nyakati nawatembelea marafiki zangu, tunazungumza, na wakati mwingine tunaimba , tunacheza mpira, tunachota maji ama kuokota kuni. Tunafanya kila kitu pamoja. Tunazungumzia kwa kawaida kuhusu shule , ama tunatembea pamoja , iwapo tunakutana , lakini pia tunarejea haraka kutoka shule, ili kwenda kuchota maji.



Chakula si kizuri kwa wengi wa watoto hawa, anasema Eva Biele mratibu wa shirika la kuwasaidia watoto kutoka Mainz nchini Ujerumani la Human Help Network nchini Ruanda.



Kuna chakula kingi cha wanga , kama mtama, muhogo, viazi vitamu na kwa kiasi kidogo ni protini. Hili mara kadhaa ndio tatizo, la watu hapa, na kwa kiasi kikubwa watoto hawafahamu kuwa protini, wanga na mafuta ni lazima katika chakula chao, ili kuweza kuwa na afya nzuri.


Jioni familia hii inakuwa pamoja. Wakati giza linaingia muda mfupi baada ya saa 12 jioni vijana hawa huingia katika nyumba yao, wanasimuliana yaliyotokea siku nzima, na wakati mwingine Rosine hunza kuimba.