1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 10 wauawa na wengine watekwa nyara Irak

1 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVZD

Si chini ya watu 10 wameuawa na darzeni kadhaa wengine wametekwa nyara,kaskazini mwa mji mkuu wa Irak,Baghdad baada ya kushambuliwa na wanamgambo wanaotuhumiwa kuwa ni wafuasi wa Al Qaeda.

Kwa mujibu wa polisi,watu wengi wamejeruhiwa na nyumba 8 zimetiwa moto katika shambulizi hilo kwenye kijiji wanakoishi Washia wengi.Wilaya ya Diyala ni miongoni mwa maeneo ya hatari kubwa nchini Irak.Wilaya hiyo pia inajulikana kama ngóme ya tawi la Al Qaeda nchini Irak.