1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Watu 17 wajeruhiwa katika shambulizi la Ukraine nchini Urusi

12 Mei 2024

Jengo moja limeporomoka katika mji wa mpakani wa Urusi, Belgorod baada ya shambulizi la Ukraine, na kusababisha kujeruhiwa kwa watu 17. Haya ni kwa mujibu wa waziri wa afya wa Urusi Mikhail Murashko.

https://p.dw.com/p/4flDG
Shambulizi la kombora Belgorod
Jengo la makaazi katika mji wa Belgorod limeharibiwa katika shambulizi la kombora linalodaiwa kurushwa na UkrainePicha: STRINGER/AFP

Wizara ya ulinzi nchini Urusi, imesema kuwa kombora la Ukraine aina ya Tochka-U, lililenga eneo la makazi mjini humo baada ya kudunguliwa na mifumo ya ulinzi wa anga.

Soma pia: Urusi yawahamisha watoto Belgorod kufuatia mashambulizi ya Ukraine

Murashko amenukuliwa na kituo cha habari cha serikali RIA Novosti akisema kwamba majeruhi hao 17 wamepelekwa kwenye vituo vya afya.

Wizara ya kukabiliana na hali za dharura imesema watu 12, wanaowajumuisha watoto wawili, wameokolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo.

Soma pia: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana

Wizara hiyo pia imeonya kuwa idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka kwa sababu sehemu ya paa la jengo hilo imeporomoka wakati maafisa wa uokoaji walipokuwa wakiwatafuta manusura.

Gavana wa Belgorod Viacheslav Gladkov amelaani mashambulizi hayo ya jeshi la Ukraine.