1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 20 wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa nchini Misri

21 Novemba 2011

Watu 20 wameuwawa na wengine zaidi kujeruhiwa kufuatia vurugu kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama zilizotokea katika uwanja wa Tahrir mjini Cairo huku uongozi wa kijeshi ukisema kadhia hiyo haitovuruga uchaguzi.

https://p.dw.com/p/13E5K
Waandamanaji mjini CairoPicha: dapd

Vikosi vya usalama vilitumia mabomu ya kutoa machozi na risasi kuzuia waandamaniji waliotaka kudhibiti boma lililopo karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani. Mamia ya waandamanaji katika uwanja wa Tahrir wamekuwa wakiushinikiza utawala wa kijeshi nchini humo kuharakisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia. Vurugu hizo zilianza pale ambapo polisi walipoyaondoa mahema ya kiasi ya waaandamanji 100 walioweka kambi katika uwanja huo baada ya maandamano ya ijumaa.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Hamidou, Ummilkheir