1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 24 wauwa kufuatia mashambulio ya mabomu Pakistan

Jane Nyingi4 Septemba 2007

Karibu watu 24 wameuawa na wengine 66 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi mawili ya bomu katika basi la kijeshi na walipuaji wa kujitoa mhanga nchini Pakistan. Hadi sasa hakuna mtu yoyote au kundi limejitokeza kuhusika na mashambulizi hayo katika wilaya iliyo na shughuli nyingi karibu na mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.

https://p.dw.com/p/CH8W
mojawapo ya misusuru ya mashambulizi ambayo yametokea Pakistan
mojawapo ya misusuru ya mashambulizi ambayo yametokea PakistanPicha: AP

Mashambilizi hayo sasa yamesababisha kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Pakistan wakati ambapo kuna joto la kisiasa kutokana na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni. Maafisa wakuu nchini humo wamedai kuwa mashambulizi hayo huenda yalifanywa na wapiganaji wa kiislamu katika harakati za kulipiza kisasi hatua ya majeshi ya pakistan kuendesha operesheni zao karibu na mpaka wa Afghanistan.

Mashambulizi hayo yaliachana kwa sekunde tu. Shambulizi la kwanza lilifanyika mapema leo katika eneo lenye usalama wa hali ya juu la Rawalpindi kusini mwa Islamabad ambalo ni makao makuu ya jeshi la Pakistan na makao rasmi ya kijeshi ya rais pervez musharaff ambaye ni rafiki mkubwa wa marekani.

Shambulizi hilo lililoharibu kabisa basi lilokuwa na wafanyikazi wa ulinzi lilitokea asubuhi wakati watu wengi wanaelekea kazini. 16 kati ya waliiokuwemo ndani ya basi hilo walifariki papohapo.Maafisa wa ukoaji ilikuwa na wakati mgumu kuwatoa majeruhi ndani ya basi hilo na kuondoa maiti.

Shambulizi la pili lilitokea karibu kilomita tatu kutoka mji uliona shughuli nyingi za kijeshi na yadaiwa uliwalenga wanajeshi waliokuwa wakienda katika makao yao makuu. Watu wanane waliuawa kufuatia shambulizi hilo.Msemaji wa kijeshi Maj generali Waheed Arshad amesema basi moja lilikuwa linamilikiwa na wizara ya ulinzi.Hata hivyo alikataa kuwataja waaathiriwa japokuwa maafisa wengine wamedai kuwa ni wanajeshi na wafanyikazi wa idara ya ujasusi.

Vikosi ya pakistan na serikali vimekabiliwa na misururu ya mashambulizi katika muda wa miezi miwili yanayolaumiwa kwa kundi la taliban na lile la al-qaeda.Mashambulizi yamekuwa jabo la kawaida nchini mpakistan tangu wanajeshi kuvamia msikiti mwekun

Zaidi ya watu 100 waliuwa baada ya msikiti huo kuzingirwa na wanajeshi wa pakistan. Maafisa wa kijeshi wanasema karibu wanajeshi 60 na wapiganaji 250 wameuawa katika mashambulizi ambayo yamechipuka wiki kadhaa zilizopita.