1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 27 wauawa Burkina Faso

Bruce Amani
11 Machi 2024

Watu 27 wameuawa katika shambulizi kwenye kijiji kimoja nchini Burkina Faso, wakiwemo wanawake na watoto.

https://p.dw.com/p/4dNyK
Ibrahim Traore wa Burkina Faso
Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Ibrahim Traore.Picha: Vladimir Smirnov/TASS/IMAGO

Mashuhuda wamesema wakaazi walikuwa wamekusanyika siku ya Ijumaa (Machi 8) kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake, wakati kundi la watu wenye silaha walipovamia kijiji cha mbali cha Tissaoghin katika mkoa wa Koulpelogo mashariki mwa nchi hiyo.

Katika wakati wa shambulizi hilo, kiongozi wa mpito Ibrahim Traore, anayeiongoza serikali ya kijeshi, alikuwa amewatembelea wanajeshi katika miji iliyo karibu ya Tenkodogo na Bagre.

Soma zaidi: Kiongozi wa kijeshi Niger afanya ziara Mali na Burkina Faso

Traore amewahimiza wanajeshi kuanzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali ambao wanaendesha harakati zao nchini humo.

Makadirio yanaonesha kuwa serikali inadhibiti tu nusu ya taifa hilo la Afrika Magharibi lenye idadi ya watu milioni 23.

Kama zilivyo nchi jirani za Mali na Niger, Burkina Faso nayo pia inatawaliwa na jeshi tangu mapinduzi ya 2022.