1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 28 wauwawa katika shambulio la bomu Syria

11 Februari 2012

Mabomu mawili yaliyotegwa katika magari yakilenga vituo vya usalama katika mji wa Aleppo yameuwa kiasi watu 28, huku waasi wakiishutumu serikali ya nchi hiyo kwa kuanzisha mashambulizi ili kuepuka lawama.

https://p.dw.com/p/141px
In this photo released by the Syrian official news agency SANA, Syrian rescue workers remove wreckage from a destroyed building at a security compound which was attacked by an explosion, in the northern city of Aleppo, Syria, on Friday Feb. 10, 2012. Two explosions targeted security compounds in the northern Syrian city of Aleppo on Friday, state media said, causing an unspecified number of casualties in a major city seen as key to President Bashar Assad's grip on power. (Foto:SANA/AP/dapd)
Shambulio la bomu dhidi ya mji wa Aleppo janaPicha: AP

Miripuko hiyo iliyotokea jana Ijumaa ilitokea wakati vifaru pamoja na vikosi vya jeshi vikisonga mbele kupambana na vikundi vya waasi katika mji ambao ni ngome kuu ya upinzani wa Homs, na wakati ambapo vikosi vya jeshi vilivyosambazwa nchi nzima vimezuwia mpango wa maandamano dhidi ya washirika wa utawala huo Urusi.

Miripuko hiyo iliyotokea majira ya karibu na mchana jana katika eneo la kibiashara la kaskazini nchini humo imewajeruhi watu 235, imesema televisheni ya taifa ya nchi hiyo, ambayo ilionyesha picha za kuogofya za watu waliojeruhiwa.

Picha za kutisha

Miili iliyovunjika vunjika ilionyeshwa ikiwa katika dimbwi la damu, nje ya majengo yaliyoharibiwa na lundo la kifusi cha mabaki ya majumba kikisambaa katika barabara kuu ya mji huo.

Televisheni ya taifa imeliita shambulio hilo la bomu ambalo ni la kwanza katika mji wa Alappo tangu vuguvugu hilo la upinzani dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad kuzuka kiasi mwaka mmoja uliopita, kuwa ni kazi ya makundi ya magaidi wenye silaha.

Televisheni hiyo imesema kuwa , mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliyekuwa katika gari iliyojazwa miripuko , ameshambulia kituo cha polisi, na kuharibu kituo cha karibu cha kusambaza chakula. Shambulio la pili lililenga kituo cha idara ya upelelezi.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio hilo nchini Syria na kusisitiza kauli yake kuwa machafuko yanayotokea nchini Syria hayana budi kukomeshwa mara moja bila kujali yanatokea upande gani.

Katibu mkuu aonya

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amerudia onyo lake kuwa mashambulio yanayofanywa na serikali ya Syria dhidi ya raia huenda yakafikia kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

epa03088377 UN Secretary-General Ban Ki-moon speaks during a joint press conference with the Palestinian Authorities President Mahmoud Abbas (unseen) in the West Bank town of Ramallah on 01 February 2012. UN Secretary-General Ban Ki-Moon kicked off a series of meetings 01 February with Israeli and Palestinian leaders, holding talks in Jerusalem with President Shimon Peres. EPA/ATEF SAFADI
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moonPicha: picture-alliance/dpa

Wakati huo huo wanadiplomasia wamesema kuwa , Saudi Arabia imesambaza rasimu ya mswada unaounga mkono mpango wa amani uliotolewa na mataifa ya Kiarabu kwa ajili ya Syria miongoni mwa wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa jana Ijumaa baada ya mswada kama huo kukataliwa kwa kupigiwa kura ya veto katika baraza la usalama wiki iliyopita na Urusi na China.

Mwandishi : Sekione Kitojo /rtre /afp

Mhariri: Pendo Ndovie