1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 285 wateuliwa kugombea Tuzo ya Amani ya Nobel

29 Februari 2024

Jumla ya wagombea 285 wameteuliwa kuwania Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4d0EX
Norway | Tuzo ya Amani ya Nobel 2023
Watoto wa Narges Mohammadi wakipokea tuzo kwa niaba ya mama yao aliyefungwa IranPicha: Javad Parsa/NTB/REUTERS

Haya yametangazwa na kamati ya tuzo hiyo ya Nobel huko Norway.

Kamati hiyo imesema wagombea hao wanajumuisha watu binafsi 196 na mashirika 89.

Hii inamaanisha kwamba idadi ya walioteuliwa mwaka huu ni ndogo ikilinganishwa na mwaka jana ambapo walioteuliwa walikuwa 351.

Idadi kubwa zaidi ya wanaowania tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2016 ambapo watu 376 walitangazwa. Kitamaduni  taasisi za Nobel huyaweka siri kwa miaka hamsini, majina ya wagombea.

Wabunge, maafisa wa serikali, marais, baadhi ya wanasayansi na washindi wa zamani wa tuzo ya Nobel, ni miongoni mwa wale wanaokubalika kuwasilisha majina ya wagombea.