1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Watu 29 wauawa katika shambulio nchini Myanmar

Tatu Karema
11 Oktoba 2023

Watu 29 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika shambulio la kijeshi kwenye kambi ya watu waliopoteza makazi yao Kaskazini mwa Myanmar

https://p.dw.com/p/4XNUq
Mazishi ya wahanga wa shambulizi dhidi ya kambi ya waliopoteza makazi Kaskazini mwa Myanmar Oktoba 10, 2023
Mazishi ya wahanga wa shambulizi dhidi ya kambi ya waliopoteza makazi Kaskazini mwa MyanmarPicha: AFP

Kanali Naw Bu wa Jeshi la Uhuru wa Kachin (KIA) ameiambia AFP kwamba shambulizi hilo la hivi karibuni, lilitokea katika saa za jioni siku ya Jumatatu. Naw Bu ameongeza kwamba walipata maiti 29 zinazojumuisha watoto na wazee .

Soma pia: Marekani kuishinikiza Myanmar kufuata njia ya demokrasia

Kanali huyo pia amesema watu 56 walijeruhiwa na kwamba wanachunguza aina ya shambulio hilo.

Utawala wa kaijeshi unachunguza ripoti hizo

Msemaji wa utawala wa kijeshi nchini humo Zaw Min Tun, amesema jeshi linachunguza ripoti hizo.

Min Tun ameongeza kuwa utawala huo wa kijeshi unaamini kuwa hifadhi ya mabomu ya waasi katika eneo hilo ndicho chanzo cha mlipuko huo, lakini hakutoa ushahidi.

Soma pia: UN yasema uhalifu wa kivita umeongezeka Myanmar

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi kuhusu mauaji hayo na kusema waliohusika lazima wawajibishwe.