1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 3 wauwawa kwenye mbio za Boston Marathon

Abdu Said Mtullya16 Aprili 2013

Mpaka sasa watu watatu wameshakufa kutokana na mashambulio ya mabomu mawili yaliyoripuka wakati wa mbio ndefu za marathon katika mji wa Boston nchini Marekani

https://p.dw.com/p/18GSI
Mashambulio ya mabomu, Boston
Mashambulio ya mabomu ,BostonPicha: picture-alliance/AP

Mabomu mawili yaliripuka kwenye mitaa iliyokuwa imejaa watu karibu na sehemu ya kumalizia mbio za marathon. Watu wasiopungua watatu wamekufa kutokana na miripuko ya mabomu hayo yaliyoutikisa mji wa Boston katika jimbo la Marekani la Massachusettes.

Jee ni magaidi tena?

Watu wengine zaidi ya140 walijeruhiwa katika kadhia ya umwagikaji wa damu. Vioo vilivunjika na sehemu za miili ya binadamu ilitapakaa- hali iliyosababisha wasiwasi kwamba magaidi wameishambulia tena Marekani. Msemaji wa Ikulu ya Marekani ambae hakutaka kutajwa kwa sababu uchunguzi bado unaendelea, ameeleza kuwa mashambulio hayo yanazingatiwa kuwa ni kazi ya magaidi.

Bombenexplosionen erschüttern Boston

Akitoa tamko juu ya mashambulio hayo Rais Obama aliepuka kutumia neno gaidi, alieleza kwamba maafisa wa Marekani hawajui ni nani aliyeyatega mabomu hayo na kwa nini. Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani alisema baadae kuwa miripuko hiyo iliyotokea kwenye mbio za marathoni zenye jadi ya miaka mingi, inazingatiwa kuwa kitendo cha ugaidi.

Obama asema aliefanya mashambulio atapatikana:

Rais Obama alilihutubia taifa kwa kuwahakikishia Wamarekani kwamba, tukio hilo litachunguzwa kwa undani. Obama alisema "Tutabainisha nani ameyafanya mashambulio haya na kwa sababu gani." Ameeleza kuwa wote wale waliohusika, au kikundi chochote- kitauona mkono mkali wa sheria. Rais Obama amesema Marekani itamjua alieyafanya mashambulio hayo.

Mabomu hayo mawili yalipishana kwa muda wa sekunde chache tu. Mwokoaji anaetoa huduma ya kwanza, amesema wanajaribu kupata damu kwa haraka. Amearifu kuwa wapo waliojeruhiwa kwa kukatika viungo vya mwili na, wengine waliumizwa na vipande vya vioo, na pote palisambaa damu.

'America stands with Boston'

Kutokana na hali hiyo ilibainika wazi kuwa shambulio la kigaidi limefanyika muda mfupi baadae polisi waliyagundua mabomu mengine mawili ambayo yalikuwa bado hayaripuka. Mamia ya watu walikuwa wamejipanga barabarani kushuhudia hatua za mwisho za mbio maarufu za marathon zinazofanyika katika mji wa Boston kila mwaka. Wakimbijaji karibu alfu 23 walikuwa wanashiriki katika mbio hizo na mara tu, walisikia miripuko mikubwa miwili na waliona moshi mkubwa na vipande vya vioo - watu wote waliwambwa na kiherehere.

Ujerumani yasikitishwa

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Guido Westerwelle, amesema ameshtushwa sana na miripuko hiyo na athari zake. "Tunawapa pole jamaa, familia na marafiki wa wahanga na tunawatakia afueni ya haraka wote waliojeruhiwa. Tukio la michezo ambalo kwa kawaida lilitakiwa kujaa utamaduni na furaha tele kwa maelfu ya wakimbiaji na mamia ya maelefu ya watazamaji kutoka Boston na ulimwenguni kote, sasa limegeuka kuwa mkosi." Westerwelle aidha amesema angependa kuona uchunguzi unafanyika haraka na waliohusika wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Außenminister Guido Westerwelle (FDP) aus Deutschland spricht am 28.01.2013 in Berlin nach der Unterzeichnung einer gemeinsamen Erklärung auf einer Pressekonferenz. Deutschland verbindet jetzt auch mit Australien eine «strategische Partnerschaft». Zwischen beiden Staaten soll es künftig eine enge Zusammenarbeit in Bereichen wie Außen- und Sicherheitspolitik, Kampf gegen Klimawandel und Energiefragen geben. Foto: Maurizio Gambarini/dpa pixel
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: picture-alliance/dpa

Mtoto pia afariki

Kwa mujibu wa taarifa za polisi mtoto aliekuwa na umri wa miaka minane alikuwa miongoni mwa waliokufa. Wahudumu wa hospitali wamearifu kwamba watu 144 walijeruhiwa 17 miongoni mwao vibaya sana.

Habari zaidi zinasema, kilometa chache kutoka kwenye sehemu ya kumalizia mbio za marathoni, pana maktaba inayoitwa "JF. Kennedy" iliyowaka moto. Lakini kamishna wa polisi ya Boston amesema huenda moto huo ulisababishwa na kifaa cha kulipuka n ahaikubainika wazi kama mkasa huo unahusiani na mashambulio ya mabomu.

Mwandishi: Schließ,Gero

Tafsiri:Mtullya Abdu

Mhariri: Josephat Charo