1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 47 wauawa katika mapigano mapya Kenya

3 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1aO

NAIROBI:

Polisi nchini Kenya wameripoti kuwa hadi watu 47 wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka nchini humo.Baadhi ya watu hao waliuawa kwa mapanga na mishale ya sumu.Vile vile mamia ya nyumba zimetiwa moto.Machafuko hayo mapya yametokea tangu aliekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan siku ya Ijumaa kutangaza mpango wa amani kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Kenya.Annan alipozungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi alisema,Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wameidhinisha ajenda ya vipengele vinne.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier akifurahia mpango huo wa amani amesema,kipaumbele ni ulinzi wa raia.Vile vile amemshukuru Annan kwa juhudi zake za upatanisho.Wakati huo huo Waziri wa Nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner amesema,pande zote mbili zilizohusika zinakabiliwa na wajibu wa kihistoria:ama wachague kujadiliana au kubeba dhamana ya maafa ya kisiasa na binadamu.

Hadi watu 900 wameuawa tangu uchaguzi wa rais wa Desemba 27 ambao Odinga na wafuasi wake wanasema umefanyiwa udanganyifu.Rais Kibaki amekanusha tuhuma hizo.